Timu ya taifa ya kriketi ya wanaume kuchuana na Uskoti

Timu ya taifa ya kriketi ya wanaume itachuana na Uskoti alasiri hii katika mechi ya ligi ya Kriketi duniani katika uwanja wa kimataifa wa Dubai.Timu hiyo inayofunzwa na Thomas Odoyo, itanuia kumaliza katika nafasi nne bora mashindanoni ili ifuzu kwa mashindano ya kombe la dunia nchini Zimbabwe, mwaka ujao. Kenya imeshinda mechi moja kati ya 12 ilizocheza katika kinyanga��anyiro hicho. Hii ni baada ya kuizidi maarifa Namibia, wiketi mbili kwa sifuri kwenye mechi ya mkondo wa pili. Timu hiyo iliandikisha sare dhidi ya timu za Milki za Kiarabu, Hong Kong, Nepal na Uholanzi wiketi moja kwa moja, kisha ikashindwa na Papua New Guinea wiketi mbili kwa bila.Kwingineko, timu ya AFC Leopards inayoshiriki katika ligi kuu ya Sportpesa humu nchini imemsajili mlinzi Yusuf Mainge kutoka timu ya shule ya upili ya Kakamega, a�?Green Commandosa�? kwa mkataba wa kipindi kirefu. Mlinzi huyo anatarajiwa kujiunga na wenzake timuni kikosi hicho kitakaporejelea mazoezi tarehe 28 mwezi huu.