Timu Ya Taifa Ya Akinadada “Malkia Strikers” Yawasili Nyumbani Leo

Timu ya taifa ya akinadada ya mpira wa wavu,a�?Malkia Strikersa�? inatarajiwa kuwasili nyumbani leo baada ya kushiriki katika mashindano ya dunia, kundi la pili nchini Ajentina na Poland.
Timu hiyo sasa imeshushwa ngazi hadi kundi la tatu baada ya kupoteza mechi zake zote za kundi la pili michuanoni. Aidha, kikosi hicho chini ya ukufunzi wa David Lunga��aho hakikushinda hata seti moja katika michuano sita dhidi ya Ajentina, Puerto Rico, Bulgaria, Poland, na Jamhuri ya Diominika. Hata hivyo, timu ya Kenya haitarejea mikono mitupu baada ya Mercy Moim kunyakua tuzo ya mfungaji bora. Mchezaji huyo anayecheza mpira wa wavu wa kulipwa nchini Finland, alijipatia alama 18 na kumpiku Tanya Acosta wa Ajentina aliyenyakua alama 11. Kocha, Lunga��aho amesema kuwa alifurahishwa na jinsi timu ilivyochea nchini Poland, kwa kuwa wakinzani wao walikuwa na mchezo wa hali ya juu.