Timu ya Raga Yashindwa na Uhispania

Matumaini ya Kenya ya Raga ya kunyakua nishani katika michezo nchini Brazil yalifyuka jana usiku; baada ya kushindwa na Uhispania alama 14 kwa 12 katika mechi yao ya nne. Timu hiyo sasa itachuana na wenyeji Brazil leo usiku A�katika mmenyano wa uorodheswaji.

Timu ya Kenya ya Raga ya wachezaji saba kila upande ilinuia kutwaa nishani katika michezo ya Olimpiki mwaka huu, hasa baada ya kufanya vyema A�kwenye msururu wa mashindano ya raga duniani kwa A�kunyakua taji ya dunia katika mkondo wa Singapore;lakini matumaini yao yaliyeyuka A�baada ya kufungwa na timu za Uingereza, New Zealand, Ujapani A�na kisha Uhispania jana usiku. Kufuatia ushinde huo, Kenya sasa imeshushwa ngazi A�na itachuana na Brazil kuwania nafasi ya 11 na 12 leo usiku. A�Wakati uo huo, mwanajudo wa pekee wa Kenya, Kiplangat Sang,ameondolewa mashindanoni baada ya kumkosea mkinzani wake Toth Krisztian raia wa Hangari, mara nne, jana usiku. Hatua hiyo ilitamausha nia ya Sang A�ya kunyakua nishani katika uzani wa kilo 90. Katika ndondi, matumaini ya A�Peter Mungai ya kutwaa nishani katika michezo hiyo yalipombojea jana usiku aliposhindwa na Argilagos Joahnys wa Kyuba robo fainali, uzani mwepesi. Mungai, alishindwa katika raundi zote tatu. Mshindi huyo sasa atamenyana na Yurberjen Martinez wa Kolombia nusu fainali kesho. A�Benson Gicharu Njagiru pia alilemewa na mpinzani chipukizi, Tsendbaatar Erdenebat wa Mongolia katika uzani wa Bantam. A�Matumaini yote ya Kenya sasa yamejikita kwa bingwa wa Afrika Rayton Okwiri, atakayejitosa ulingoni kesho dhidi ya Mohammed Rabii A�wa Moroko, katika pigano la robo fainali, uzani wa Welter.