Timu ya Kenya ya mbio za masafa yashiriki katika mbio katika michezo ya Jumuiya ya madola

Timu ya Kenya ya mbio za masafa ya kadiri na wachomokaji itakayoshiriki katika michezo ya Jumuiya ya Madola inafanya mazoezi katika msitu wa Karura na uwanjani Kasarani mtawalia.

Huku takriban majuma matatu yakisalia ili michezo ya Jumuiya ya madola inga��oe nanga jijini Gold Coast, Australia, timu ya Kenya imeimarisha mazoezi yake huku ikinuia kuendeleza msururu wa matokeo mazuri katika riadha.Mshindi wa nishani ya fedha katika mbio za mita mia nne Barani Afrika Alex Sampao ameelezea imani yake kuwa atanyakua nishani ya dhahabu, hii ikiwa ni mara yake ya kwanza kushiriki kwenye michezo hii.A�Bingwa wa mbio za chipukizi duniani na katika michezo ya Jumuiya ya madola kwenye mbio za mita 1,500 Kumari Taki, aliyejiunga na timu ya wanariadha wazoefu ameapa kuiga mfano wa wanariadha hao huku akinuia kuonesha mchezo wa kuvutia. A�Michezo ya mwaka huu itaandaliwa kuanzia tarehe nne hadi tarehe kumi na tano mwezi Aprili jijini Gold Coast Australia. Wakati wa michezo ya mwaka 2014, Kenya ilimaliza katika nafasi ya kwanza kwenye msururu wa medali kitengo cha riadha baada ya kunyakua nishani kumi za dhahabu, kumi za fedha na tano za shaba.