Timu Ya Harambee Starlets Yaanza Mandalizi Ya CECAFA

Harambee_Starlets_photo_by_Soccer_Embassy[2]T

Timu ya Harambee Starlets, imeshuka nafasi mbili, kutoka 130 hadi 132 katika orodha ya shirikisho la soka ya akinadada duniani.Hii ni baada ya kushiriki katika mashindano nchini Uhispania walikoalikwa kwa muda wa juma, mwezi huu.

Aidha, timu hii imeanza maandalizi ya mashindano baina ya mataifa ya Afrika Mashariki na Kati CECAFA, yatakayoandaliwa nchini Uganda mwezi ujao. Licha ya kuishinda Cresten Cranes ya Uganda, katika mechi ya kirafiki, kabla ya kuelekea nchini Uhispania, Starlets ingali nafasi tatu chini ya majirani hao na inaorodheshwa ya 25 huku Naijeria A�ni ya kwanza Barani Afrika na ni ya 37 duniani; ikifuatiwa na Ghana katika nafasi ya pili, A�na nafasi ya 46 duniani.

Kameruni inashikilia nafasi ya tatu na ya 47 duniani. Ethiopia inaongoza katika eneo la Afrika Mashariki huku ikiwa katika nafasi ya 105 duniani nayo Tanzania ni ya pili katika nafasi ya 125. Marekani inaongoza duniani ikifuatwa na Ujerumani na Ufaransa katika nafasi za pili na tatu mtawalia. Orodha ijayo ya shirikisho la soka duniani itatolewa mwezi Disemba.