Timu ya Chelsea kukosa huduma za wachezaji muhimu kwenye kombe la kilabu bingwa Barani Ulaya

Timu ya Chelsea inayoshiriki katika ligi kuu ya soka nchini Uingereza itazikosa huduma za wachezaji waliojeruhiwa David Luiz, Tiemoe Bakayoko na Ross Barkley huku timu hiyo ikiwaalika miamba wa soka nchini Uhispania Baselona uwanjani Stamford Bridge kwa mechi ya kuwania kombe la kilabu bingwa Barani Ulaya, leo usiku. Hata hivyo, Marcos Alonso anatarajiwa kurejea timuni baada ya kutoichezea ChelseaA� mechi mbili za mwisho. Baselona ilimjumwisha mlinzi Gerard Pique mwishoni mwa juma lililopita na sasa huenda pia atajumwishwa kikosini. Thomas Vermaelen aliyetarajiwa kukosa kushiriki mchuanoni amejumwishwaA� lakini Nelson Semedo anahudumia marufuku. Chelsea na Baselona zimechuana kwenye kombe hili mara 12 tangu mwaka 2000. Mara ya mwisho timu hizi kucheza ilikuwa msimu wa mwaka 2011-12, nusu fainalini. Aidha, Chelsea imeshinda mara nne, Baselona mara tatu na kutoka sareA� mara tano.