Timu ya Baselona yawatunuku waathiriwa wa shambuliza la kigaidi jijini Baselona

Timu ya Baselona inayoshiriki katika ligi kuu ya soka nchini Uhispania, imewatunuku waathiriwa wa shambulizi la kigaidi jijini Baselona juma lililopita, ushindi wa mabao mawili kwa bila dhidi ya Real Betis. Wachezaji hao walijumwika kwa muda wa dakika moja kabla ya mechi kunga��oa nanga na kutoa heshima zao za mwisho kwa waathiriwa. Baselona ilianza kufunga kwanza baada ya Gerard Deulofeu kujifunga, Alin Tosca alipoubetua mkwaju. Deulofeu aliisaidia Baselona kutinga bao la pili baada ya kumwandalia pasi Sergi Roberto aliyetikisa wavu kwa mkwaju waA� penalti. Wakati uo huo, Real Madrid ilinyakua ushindi wa mabao matatu kwa sufuri dhidi ya Deportivo La Coruna, baada ya Gareth Bale, Casemiro na Toni Kross kutikisa wavu. Athletic Bilabao ilitoka sare tasa na Getafe.