Timu ya Asenali kukichezesha kikosi hafifu wakichuana na Bate Borisov leo usiku

Timu ya Asenali inayoshiriki katika ligi kuu ya soka nchini Uingereza, inanuia kukichezesha kikosi hafifu kwenye mechi ya kuwania kombe la a�?Yuropaa�? dhidi yaA� Bate Borisov leo usiku. Laurent Koscielny, Mesut Ozil na Alexis Sanchez ni miongoni mwa wachezaji mahiri ambao huenda wasicheze mchuano huo. Mchezaji aliyesajiliwa msimu huu, Alexandre Lacazette na Sead Kolasinac huenda pia wakakosekana. Danny Welbeck hatacheza mechi hiyo kwani anauguza jeraha huku Asenali ikinuia kuendeleza msururu wa matokeo bora baada yaA� kuilemea Cologne mabao matatu kwa moja katika mchuano wa kwanza.