THIWASCO yakanusha madai ya kusambaza maji inayoeneza virusi vya Rota kwa watoto

Kampuni ya huduma za maji ya Thika-THIWASCO imekanusha madai kwamba kuzuka kwa virusi vya Rota miongoni mwa watoto katika kaunti ndogo ya Thika kumetokana na mfumo wake wa usambazaji maji. Kampuni hiyo ya maji ilisema ilipata habari kuhusu kuzuka kwa virusi hivyo kupitia mitandao ya kijamii baada ya shule kadhaa katika eneo hilo kuathiriwa na wanafunzi kupokea matibabu.A� Kulingana na mkurugenzi mkuu wa kampuni hiyo, Moses Kinya, kitengo cha usafishaji maji cha kampuni hiyo kilichukua hatua haraka na kuchunguza maji yake kuhakikisha hayana vijidudu.A� Alisema kampuni hiyo hutibu maji kila siku kwa kutumia kemikali mbali mbali ikiwemo dawa ya klorini na gesi ambayo huchuja na kuondoa vijidudu vinavyoonekana na visivyoonekana kulingana na viwango vya shirika la afya duniani. Aliwahakikishia wateja wao kwamba maji yake yameafikia viwango vya ubora. Alitoa wito kwa wale wanaotumia maji ya visima au kununua kutoka wa wachuuzi wa maji kuhakikisha wameyachemsha kwani si safi ya kunywa.