Tetemeko la ardhi yasababisha maafa Iran

Tetemeko kubwa la ardhi lenye makali yaA� 7.3 kwenye mizani ya Richa limetikisa eneo la kaskazini la Iran linalopakana naA� Iraq na kusababisha maafa.Kwa mujibu wa ripoti za mashirika ya kutoa misaada,takriban watu 61 wamefariki dunia kutokana na janga hilo la asili ,huku wengine 300 wakisemekanaA� wamejeruhiwa vibaya,magharibi mwa Iran huku wanne wakiripotiwa kufariki dunia katika nchi jirani ya Iraq.

Idadi ya waliofariki dunia huenda ikaongezeka,huku wakazi wa maeneo hayo wakitoroka makazi yao hadi kwenye barabara kutokana na taharuki.Misikiti katika mji mkuu wa Iraq ,BaghdadA� imekuwa ikiendesha sala kwa waathiriwa kupitia vikuzasauti.Wengi wa waliofariki dunia walikuwa katika mji wa Sarpol-e Zahab,kulingana na mshirikishi mkuu wa huduma za dharura Pir Hossein Koolivard.Uharibifu uliripotiwa kutokea katika vijiji vinane.Morteza Salim wa shirika la mwezi mwekundi la Iran alithibitisha jambo hilo.Hata hivyo imesemekana juhudi za uokozi zinatatizwa na maporomoko ya ardhi.