Tetemeko la ardhi nchini Taiwan lasababisha vifo vya takriban watu wawili

Maafisa wa serikali nchini Taiwan wamesema kuwa tetemeko kubwa la ardhi nchini humo limesababisha vifo vya takriban watu wawili na kujeruhiwa kwa wengine zaidi ya 200. Tetemeko hilo la 6.4 katika kipimo cha ritcher lilitokea mwendo wa saa tano na nusu usiku takriban kilomita A�20 katika pwani ya Kusini Mashariki . A�Takriban watu 150 wameokolewa kutoka nyumba zao na hoteli ambazo zimeporomoka katika mji wa A�Hualien. Picha zinaonyesha majengo yalioegemea upande mmoja , vifusi vilivyotawanyika A�na uharibifu mkubwa katika barabara za sehemu hiyo . Vyombo vya habari katika eneo hilo vimeripoti kuwa miongoni mwa majengo yalioharibika vibaya ni hospitali . Takriban nyumba elfu 40 hazina maji na barabara kuu pamoja na vivukio zimefungwa . wakazi wameambiwa kutorejea katika nyumba zao zilizoharibika na takriban watu A�800 wametafuta hifadhi katika majengo ya kijmaii. Afisi na shule katika eneo hilo zitafungwa hadi siku ya Jumatano huku jeshi likiitwa kutoa usaidizi katika hali za dharura . A�Mji wa Hualien una takriban wakazi A�100,000 na ni kituo maarufu cha utalii.