Tetemeko la ardhi lasababisha vifo vya zaidi ya watu 130 nchini Mexico

Tetemeko kubwa la ardhi limekumba eneo la katikati A�la nchi ya Mexico na kuisababisha vifo vya zaidi ya watu 130 na kuporomosha manyumba kadhaa katika mji mkuu Mexico City. Waokoaji wanawatafuta manusura, huku ikiripotiwa kuwa watoto wa shule wamenaswa kwenye jengo la shule yao lililoporomoka kutokana na A�janga hilo.Tetemeko hilo la ardhi lenye makali ya 7.1 kwenye mizani ya Richa limesababisha uharibifu mkubwa katika majimbo ya Morelos na Puebla na vile vile jimbo la Mexico. Janga hilo lilitokea huku wakazi wa sehemu hiyo wakifanya mazoezi ya kujinusuru kutokana na tetemeko la ardhi,miaka 2 tangu kulipotokea tetemeko la ardhi A�lililosababisha vifo vya maelfu ya watu miaka 32 iliopita. Mexico mara kwa mara hukumbwa na mitetemeko ya ardhi. Mapema mwezi huu tetemeko la ardhi lenye makali ya 8.1 kwenye mizani ya Richa lilitokea kusini mwa nchi hiyo na kusababisha vifo vya watu 90. Kitovu cha tetemeko la leo kilikuwa karibu na Atencingo katika jimbo la Puebla, umbali wa kilomita kutoka mji mkuu Mexico City na lilitokea kwenye kina cha A�kilomita 51 kwa mujibu wa kituo cha A�kuchunguza majanga ya mitetemeko ya ardhi. Iliarifiwa kuwa A�zaidi ya watu 64 wamefariki dunia A�katika jimbo la Morelos na wengine 29 katika jimbo la Puebla. Vifo vya watu 36 vimeripotiwa katika mji mkuu A�Mexico City.