Tetemeko la ardhi lasababisha kifo nchini Italia

Tetemeko  la ardhi lililofikia kipimo cha nukta 4 kwnye mizani ya Richa kimekumba kisiwa cha Ischia, kwenye mwambao wa mji wa Naples huko Italia na kusababisha kifo cha mtu mmoja  na kuwajeruhi wengine 2, huku majumba kadhaa yakiripotiwa kuporomoka. Wakazi na watalii walikimbilia usalama kwenye barabara za kisiwa hicho kinachopendwa na watalii. Picha za runinga  zilionesha takriban majumba sita yaliporomoka katika mji wa Casamicciola, likiwemo kanisa moja wakati wa  tetemeko hilo la ardhi mwendo wa saa mbili na dakika 57 za usiku. Taasisi ya kitaifa ya  utafiti wa maswala ya volcano ilithibitisha kuwa tetemeko hilo lilikuwa na makali ya nukta 4. Afisa kutoka idara ya usalama wa raia Giovani Vittozi alisema kuwa mwanamke mmoja alifariki dunia baada ya kuporomokewa na samani katika  kanisa moja, huku maafisa wa serikali wakiendelea kutafuta manusura wa mkasa huo.