Ted Cruz asitisha Kampeni Za kuwania Urais katika Chama Cha Republican Na Kumwachia Trump

Ted Cruz ametangaza kusitisha kampeini zake za kuwania tiketi ya urais ya chama cha A�A�Republican baada ya kushindwa vibaya na mkwasi Donald Trump katika shughuli ya uteuzi ya eneo la Indiana. Trump ambaye hapendelewi na wengi wa wanachama wa chama chake, sasa ana uhakika wa kushinda tiketi ya chama hicho. Awali Cruz alikuwa amemtaja Trumph kuwa mtu asiyeaminika na asiyestahili kuiongoza Marekani. Kinyanga��anyiro cha tiketi ya chama cha Democratic ni kati ya A�Hillary Clinton na Bernie Sanders.