Tanzania kushirikiana na wasanii wa Pokot kutayarisha senema

Waigizaji mashuhuri wa filamu kutoka nchini Tanzania wanashirikiana na wasanii wa Pokot Magharibi katika kutayarisha senema ambapo mamia ya vijana wa eneo hilo wataajiriwa kucheza senema.Wakiongea wakati wa uzinduzi wa filamu ya kwanza kwa jina a�?Riziki Yangua��, wasanii hao wa hapa nchini walisema wanafurahia changamoto zinazowakumba vijana wa eneo hilo.Ashiono Awendo na Sammy Abuyanza alisema wanataka kuonyesha sura nzuri ya pokot Magharibi na kuwaelimisha vijana kuhusu athari za tabia mbaya kama vile matumizi ya mihadarati na ukimwi.Mcheza senema na mwanasarakasi maarufu wa Tanzania Rashid Munshehe, AKA, Kingwendu alisema waliafikia makubaliano na wamefanikiwa kukuza vipaji vya vijana wa Pokot Magharibi.Gavana John Lonyangapuo alisema atajenga ukumbi wa senema mjini humo ili kuwavutia watazamaji senema kutoka nje.