Tamasha Za Kitamaduni Za Bi.Mrembo Zatarajiwa Kuandaliwa Kampala ,Uganda mwaka ujao

Makala ya tatu ya kila miaka miwili ya tamasha za kitamaduni za Bi. Mrembo miongoni mwa mataifa wanachama wa jumuiya ya Afrika mashariki yataandaliwa mjini Kampala ,Uganda mwaka ujao. Tamasha hizo ambazo zitakuwa mwenyeji wa Bi. Warembo watano bora miongoni mwa mataifa sita wanachama wa jumuiya hiyo zitaangazia tamaduni mbali mbali za kanda hii kama njia moja ya kuimarisha utangamano wa kijamii mbali na kubadilishana maoni na maarifa miongoni mwa mataifa wanachama. Nchi hii iliandaa makala ya pili ya tamasha za Jumuiya Ya Mashariki Utamaduni-JAMAFEST mwaka jana jijini Nairobi, huku washiriki kutoka mataifa yote wanachama wakihudhuria. Afisa anayehusika na tamasha hizo za Bi. Mrembo katika eneo la Afrika mashariki, Ignatius Wafula, alisema lengo la halfa hiyo na kuimarisha na kupanua shughuli za kiuchumi, kisiasa, kijamii na kitamaduni miongoni mwa mataifa wanachama kwa lengo la kuinua hali ya maisha ya watu wa kanda hii kupitia ushindani, uzalishaji ulioongezwa dhamana, biashara na uwekezaji.
Wafula anasema kaunti ya Turkana ina mipango ya kuandaa tamasha zake mwezi ujao ikifuatiwa na kaunti za Kisumu, Bungoma, Mombasa na Nyeri baadaye.