Tamasha Ya ‘Project X’ Yaendelea Kuzua Utata

Mkurugenzi mkuu wa Halmashauri ya kuorodhesha filamu hapa nchini, Ezekiel Mutua amekashfu vikali tamasha lililopangwa la vijana kwa jina Project X ambalo litaandaliwa mtaani Kileleshwa tarehe-12 mwezi huu. Mutua amewataka wananchi kutoa habari kuhusu tamasha hilo la mahaba linalokaidi maadili na kuhimiza uraibu wa mhadarati, ngono na utayarishaji filamu za kutia ashiki. Mutua alisema tamasha hilo al-maarufuA�a�?Project Xa�� ni njama ya baadhi ya wafanyabiashara ambao wananuia kutumia fursa ya kutengeneza filamu za ngono. Tamasha hilo limepatiwa jina la filamu za Hollywood zilizotengenezwa mwaka 2012 ambazo zimejikita katika maadhimisho ya siku ya kuzaliwa ambapo wahusika hutumia mihadarati na kujihusisha maswala ya ngonoA�kiholela. Bodi ya kuorodhesha filamu hapa nchini imesema iko macho na imewaonyaA�waandalizi wa tamasha hilo kuwa watachukuliwa hatua za sheria.