Wakenya Milioni 2 Wamo Katika Hatari Ya Kukumbwa Na Baa La Njaa

Takriban wakenya milioni mbili wanakabiliwa na hatari ya kukumbwa na baa la njaa kutokana na hali ya ukame inayokithiri nchini. Waziri wa ugatuziA� Mwangi KiunjuriA� alisema kufeli kwa mvua ya mvuli katika miezi ya November na December kumechangia pakubwa hali hiyo.Akiongea wakati wa mkutano wa mawaziri,Kiunjuri alisema hali hiyoA� imekithiri kiwango cha kushuhudiwa katika maeneo ambayo nchi hii imekuwa ikitegemea kwa chakula.Waziri huyo aliongeza kuwa mifugo ndio walioathirika pakubwa.

Akiongea,waziri wa maji Eugene Wamalwa ametoa wito kwa wanasiasa kuunga mkono miradi ya maji inayotekelezwa na serikali inayolenga kutoa suluhu ya muda mrefu kwa matatizo ya uhaba wa maji yanayowakumba wengi.

Wakati huo huo,wizara ya ugatuzi ikishirikiana na idara ya ustawi wa kimaendeleo ya Uingereza inasambaza msaada wa kifedha kwa takriban familia 97,000 kwenye kaunti zilizoathirika na ukame huo kuzisaidia kununua chakula. Serikali imesema kuna chakula cha kutosha kwenye maghala yake ya nafaka.