Takriban Wasichana 9,000 Wapata Mimba Busia

Takriban visa 9,161 vya wasichana wadogo kupata mimba vimeripotiwa katika kaunti ya Busia tangu mwezi Januari hadi Novemba mwaka huu. Cha kushangaza ni kwamba takwimu zinaonyesha kuwa zaidi ya wasichana 214 wa umri wa kati ya miaka 10 hadi 14 ni miongoni mwa wale wanaoshika mimba. Miongoni mwao hupata mimba na kuacha shule na kuolewa. Afisa mkuu wa kimatibabu katika kaunti ya Busia Assumpta Matekwa, amesema kuwa shughuli za kijamii zinazotekelezwa wakati wa likizo na mwishoni mwa juma katika kaunti hiyo miongoni mwa maswala mengine husababisha tatizo hilo. Alionya kwamba hali ya wasichana wa umri mdogo kupata mimba na kuolewa huenda ikaendelea iwapo haitathibitiwa.