Takriban wafungwa 100 watoroka kwenye gereza moja nchini Ivory Coast

Maafisa nchini Ivory CoastA� wamesema kuwa mlinzi mmoja huenda aliruhusu takriban wafungwa-100 kutoroka kwenye gereza moja nchini humo. Coulibaly Ouamien ambaye ni naibu meya wa mji wa Katiola ambako kisa hicho kilitokea amesema gereza hilo linazingiriwa na ukuta thabiti, mbali na kuwa na milango kadhaa, hivyo basi wafungwa hao walisaidiwa kutoroka.A� Inasemekana kuwa lango la gereza hilo lilikuwa limefunguliwa. Wafungwa-36 walikamatwa huku walinzi wa gereza hilo wakifutwa kazi kufuatia kisa hicho.