Takriban Raia 18 Wauawa Kwenye Mashambulizi Ya Angani Raqa, Syria

Wanaharakati nchini Syria wamesema kuwa takriban raia A�18 A�wameuawa kwenye mashambulizi ya angani katika mji wa Raqa,ambao ni makao makuu ya A�wanamgambo wa Islamic State. Mamia ya raia walijeruhiwa kwenye mashambulizi hayo, kwa mujibu wa shirika moja la Syria la kutetea haki za binadamu lenye makao makuu yake nchini Uingereza. Shirika hilo limesema halikuweza kubaini ni nani aliyetekeleza mshambulizi hayo,japo shirika lingine lilishutumu ndege za Russia. Mji wa Raqqa ulishambuliwa tena na ndege za kivita za kikosi cha kimataifa kinachoongozwa na Marekani. Hapakuwa na habari A�kamili kuhusu hasara wala vifo kutokana na mashambulizi hayo. Kombora moja liliangukia jengo moja katika mji huo.