Takriban makanisa 700 yamefungwa nchini Rwanda

Takriban makanisa 700 yamefungwa nchini Rwanda kwa kutoafiki sheria za ujenzi  na bughudha ya makelele.Nyingi ya kanisa hizo ndogo ni za kipentekoste.Kulingana na afisa mmoja wa serikali Justus  Kangwagye,kile ambacho zinahitajika kufanya ni  kuafikia viwango vilivyowekwa vya kutotumia vipiza sauti vya nguvu kuwavutia waumini.Badhi ya makanisa hayo ilisemekana yamekuwa yakiendesha ibaada bila vibali.Kulingana na sheria mpya za nchi hiyo wahubiri wote sharti wawe wamefuzu mafunzo ya  kithiolojia kabla ya kufungua makanisa.Iliarifiwa kuwa operesheni hiyo ilifanywa na vyombo vya utawala vya sehemu husika kwa ushirikiano na bodi ya utawala ya Rwanda.