Taharuki Yatanda Kufuatia Mauaji Ya Watu Wawili Kerio

Taharuki bado imetanda huko Kinyach katika eneo la bonde la A�Kerio kufuatia mauaji ya watu wawili baada ya makabiliano baina ya jamii mbili kuhusu lishe na maji kwa mifugo wao.Kisa hicho kilisababisha mauaji ya mama mmoja wa watoto wanne na mwanamme mmoja kwenye daraja moja linalounganisha kaunti za A�Baringo A�na Elgeyo-Marakwet A�na kuzua tahamaki.Kulingana na mtua aliyeshuhudia kisa hicho,idadi ya mifugo isyojulikana pia waliibiwa na kuelekezwa upande wa kaunti ya Pokot.Akidhibitisha kisa hicho,chifu wa lokesheni ya Kinyach alisema taharuki imekuwa ikitanda katika sehemu hiyo huku athari za A�kiangazi zikikithiri katika sehemu hiyo.Aliongeza kwamba mifugo pia wanaendelea kuangamia katika sehemu hiyo na akatoa wito kwa serikali ya kitaifa kuingilia kati na kutoa lishe kwa wanyama pamoja na maji kwa raia wa sehemu hiyo.