Syria Yaidhinisha Msaada Kwa Maeneo Yaliyokubwa Na Vita

Serikali ya Syria imeidhinisha kupelekwa kwa misaada ya kibanadamu katika maeneo saba yanayoaminika kukumbwa na mapigano.A� Kwa mujibu wa mjumbe maalum wa umoja wa mataifa nchini Syria, Staffan de Mistura, baada ya kufanyika kwa mazungumzo jijini Damascus hapo jana, serikali ya Syria imekubali kuwa ina jukumu la kufanikisha au kuruhusu misaada ya kibinadamu kufika maeneo yote nchini humo. Misafara ilikuwa ikijiandaa kuondoka kupeleka misaada katika maeneo yanayoathirika. Hata hivyo rais waA� Syria Bashar al-Assad alitilia shaka mkataba huo wa kusitisha mapigano kwa vile pande hizo zote hazitaacha kutumia silaha.