Staffan de Mistura Aimiza Marekani na Urusi Kuingilia Kati Kuokoa Mazungumzo ya Amani

Mjumbe wa Umoja wa mataifa huko Syria Staffan de Mistura amezihimiza Marekani na Urusi kuingilia kati katika ngazi ya juu kuokoa mazungumzo ya amani.

Akiongea baada ya kulifahamisha baraza la usalama la Umoja wa mataifa kuhusu mpango huo wa amani Staffan de Mistura alisema makubaliano ya kusitisha mapigano hapo mwezi Februari bado yanazingatiwa.

Ghasia huko Syria zimeendelea katika siku za hivi karibuni licha ya kuwepo kwa hatua ya kukomesha vita. Raia 20 waliripotowa kuuawa kufuatia mashambulizi ya anga yaliyotekelezwa na vikosi vya serikali dhidi ya hospitali moja na jingo moja la makazi mashariki mwa eneo la Aleppo.

Waliouawa ni pamoja na watoto na daktari wa pekee wa magonjwa ya watoto katika eneo hilo. Ongezeko la mapigano katika jiji hilo kubwa la Syria limeshuhudiwa hu

ku taarifa zikiibuka kwamba vikosi vya serikali vinavyoungwa mkono na ndege za kivita za Urusi vinatejkelezwa mashambulizi makubwa.