Staa wa Juventus Gonzalo Higuain apachika bao 2

Kimataifa,A�A�timu ya Juventus ya ItaliaA�A�inakaribia kufuzu kwa fainali yake ya pili ya ligi ya mabingwa Barani Ulaya, katika kipindi cha misimu mitatu baada ya Gonzalo Higuain kufunga mabao mawili huku timu hiyo ikiishindaA�A�Monaco kwenye mechi ya mkondo wa kwanza ya nusu fainali.

Monaco ilianza vyema mechi hiyo huku mshambulizi mahiri Kylian MbappeA�A�akimlazimu mlindalango Gianluigi Buffon kufanya kazi ya ziada.A�A�Hata hivyo, Higuain aliifungia Juventus bao la kwanza alipounganisha krosi ya kisigino kutoka kwa mlinzi Dani Alves. Radamel Falcao nusura aifungie Monaco baada ya kipindi cha pili kuanza kisha Higuain akaifungiaA�A�A�Juventus bao la pili. Baada ya Real Madrid kuishinda Atletico Madrid siku ya Jumanne, kwenye nusu fainali nyingine, huenda yakawa marudio ya fainali ya mwaka 1998 ambapo Madrid aliishinda Juventus bao moja kwa sifuri na kuibuka washindi.