SRC yapunguza mishahara ya watumishi wa umma

Tume ya mishahara na marupurupu SRC imepunguza mishahara ya watumishi wa umma akiwemo rais na kufutilia mbali marupurupu ya vikao na usafiri ya wabunge . Kwenye muundo huo mpya wa mishahara uliotangazwa leo , rais atapata mshahara wa shilingi milioni 1.44 kila mwezi kutoka shilingi milioni 1.65, naibu rais atapata mshahara wa shilingi milioni 1.22 kutoka shilingi milioniA� 1.4 alizokuwa akilipwa. Magavana watalipwa shilingi A�924,000 kutoka shilingiA� milioni 1.056, huku manaibu wao wakipata shilingiA� 621,250 kutoka shilingi 701,441 . Wanachama wa mabunge ya kaunti watapokea mishahara ya shilingiA� 144,000 kila mwezi kutoka shilingi 165,000 . Mishahara ya mawaziri itakuwa shilingi 924,000 huku maspika wa mabunge yote mawili wakipata mishahara ya shilingi 1,155,00,mishahara ya makatibu wa wizara pia imepunguzwa kutoka shiligiA� 874, 500 hadi shilingi A�765, 188A� . Katika kutayarisha mundo huo mpya wa malipo , tume ya SRC pia imefutilia mbali marupurupu ya vikao na majukumu maalum ya wabunge wa mabunge ya taifa na seneti na pia marupurupu ya usafiri. Mwenyekiti wa tume hiyo Sarah Serem amesema muundo huo mpya wa mishahara ambao unalenga kupunguza gharama ya mishahara ya watumishi wa umma kwa shilingi bilioni 8.8 kila mwaka utaanza kutekelezwa wakati maafisa wa serikali wa bunge la 12 watakapoapishwa.