Sportpesa yasajili Marvin Onyango wa timu ya Ushuru

Timu ya Wazito, iliyopandishwa ngazi hadi ligi kuu ya Sportpesa, imemsajili mlinzi Marvin Onyango kutoka timu ya Ushuru.Timu hiyo inayofunzwa na Frank Ouna inaimarisha kikosi chake huku ikijiandaa kushiriki katika ligi kuu humu nchini kwa mara ya kwanza, na imemsajili Onyango kutoka Ushuru, itakayoshiriki katika ligi ya taifa kwa mara nyingine baada ya kushindwa na Thika United katika mechi ya mchujo.

Kwingineko, mkufunzi wa Manchester City Pep Guardiola atanuia kushinda mechi ya 18 mfululizo ligini dhidi ya Newcastle United baadaye leo uwanjani St James. Mzaliwa huyo wa Uhispania tayari ameweka rekodi nchini Uingereza kwa kushinda mechi 17 mfululizo, rekodi bora ikilinganishwa na mechi 16 alizoshinda akiifunza Barcelona. Aidha Guardiola sasa anaangazia kuvunja rekodi ya ushindi wa mechi 19 aliyoweka na timu ya Bayern Munich, ikiwa rekodi bora zaidi katika ligi kuu za Bundesliga, Uingereza, La Liga, Serie A na Ligue 1, kwa kuandikisha ushindi dhidi ya Newcastle.