Spika wa Senate Kenneth Lusaka ahimiza masenata kutekeleza majukumu yao

Spika wa bunge la Senate Kenneth Lusaka, amewahimiza maseneta kutekeleza jukumu lao na kutathmini utendakazi wa serikali za magatuzi kulingana na sheria na wajiepushe na uonevu na kuwakandamiza magavana. Akiongea wakati wa A�kuwafahamisha maseneta taratibu za bunge katika hoteli moja ya Naivasha, Lusaka alisema maseneta wa bunge lililopita walitumia vibaya nyadhifa zao na kuibua madai mbali mbali dhidi ya magavana. Lusaka alisema seneti ya kwanza ilikumbwa na unga��anga��aniaji mamlaka kati ya maseneta na baadhi ya magavana ambao walilaumiwa kwa kutumia vibaya fedha za kaunti. Lusaka alisema maseneta wengi kwenye bunge la kwanza la seneti walikosa uwajibikaji kwenye jukumu lao la utathmini kwani walikuwa wanataka kuwania nyadhifa za ugavana. Lusaka ambaye alikuwa gavana wa Bungoma alipendekeza kwamba utaratibu wa kuwaondoa magavana ndio wapasaa kuwa hatua ya mwisho kwani utaratibu huo umetumiwa vibaya na baadhi ya wanasiasa. Spika huyo aliwaambia maseneta kuhakikisha kwamba wakati wowote wanapomuagiza gavana kufika mbele yao kwa mahojiano, hakupaswi kuwa na hila fulani bali liwe ni zoezi mahususi la uwajibikaji.