Spika wa Bunge la taifa Justin Muturi ataka uteuzi wa haraka kwa wanachama

Spika wa bunge la taifa Justin Muturi ameitaka kamati mpya ya uteuzi kuharakisha kuteuwa wanachama wa kamati mbali mbali ili kudumisha shughuli za bunge. Akihutubia bunge baada ya kuidhinishwa kwa kamati ya wanachama 19, Muturi alisema ipo haja ya kamati hiyo kuandaa mkutano wake wa kwanza ili kusaidia bunge kutekeleza shughuli zake. Wakati huo huo kiongozi wa wengi katika bunge la taifaA�Aden Duale na kiongozi wa wachacheA�John Mbadi wamethibitisha kuwa uanachama wa kamati hiyo ya uteuzi uliafikiwa baada ya mashauriano ya kina.

Huku Duale akiwataka wabunge kujifahamisha kuhusu kanuni za bunge, Mbadi alisema ipo haja ya kubuniwa dharura kwa kamati mbali mbali ili kushughulikia maswala kadhaa nchini. Ametaja visa ambapo maafisa wa polisi wametumia nguvu kupita kiasi dhidi ya waandamanaji hali iliyosababisha vifo na majeraha.

Mbadi amesema nafasi ya kidemokrasia imepungua huku uhuru wa kuongea na kujielezea ukididimia na kwamba bunge halifai kuwa kiungo cha afisi ya rais. Mbunge waA�Suba Kusini pia amewataka wabunge wapya kutetea maadili ya vyama vilivyowadhamini katika uchaguzi mkuu. Spika Justin Muturi alimhakikishia mamlaka ya kuwachukulia hatua wabunge yako mikononi mwa vyama vya kisiasa.