Spika Aitisha Kikao Kingine Cha Bunge

Spika wa bunge la taifa, Justin Muturi ameitisha kikao kingine maalum cha bunge kiandaliwe kesho ili kuwezesha wabunge kukamilisha mjadala kuhusu marekebisho ya sheria za uchaguzi baada ya kikao cha hapo jana kukumbwa na mkanganyiko. Katika arifa ya gazeti rasmi la serikali iliyotolewa jana usiku, spika huyo alisema kutakuwa na vikao viwili kimoja asubuhi na kingine wakati wa jioni. Kikao hicho maalum kiliitishwa kujadilia swala hilo baada ya mjadala huo kutatizwa jana jioni. Wabunge wa upinzani waliwashutumu wenzao wa Jubilee kwa kujaribu kuhujumu sheria za uchaguzi ili kuzindua mfumo wa kawaida wa upigaji kura. Wabunge wa mrengo wa CORD wamedai kwamba sheria ya mwaka 2016 kuhusu marekebisho ya sheria za uchaguzi ni sheria inayoweza kujadiliwa kwaniilipitishwa baada ya mrengo wa upinzani na ule tawala kukubaliana kuipitisha bila kuifanyia marekebisho. A�