South B United yafuzu kwa nusu fainali

Timu ya a�?South B Uniteda�� ilifuzu ya kwanza kwa nusu fainali ya mashindano ya soka ya Kothbiro baada ya kuishinda a�?Pumwani All Starsa�� bao moja kwa bila katika robo fainali ya kwanza iliyochezwa jana uwanjani Ziwani. Timu hizo mbili zilitoshana nguvu katika kipindi cha kwanza kabla ya Abraham Dawo kuifungia a�?South Ba�� bao la ushindi katika dakika ya 74 huku ikifuzu kwa nusu fainali pamoja na Beirut FC iliyoishinda Umeme Bees mabao 5-4 kwa njia ya penalty. Mechi hiyo ilimalizika sare bao moja kwa moja. Robo fainali mbili zitachezwa leo ambapo a�?Kingstonea�� itachuana na a�?Fifa Besta�� nayo a�?Masaa�� ipambane na a�?Gaa-Hurumaa��. Awamu ya nusu fainali itaandaliwa tarehe 29 na 30 mwezi huu huku mechi ya kutafuta timu ya tatu ikichezwa tarehe sita mwezi January. Fainali itachezwa tarehe saba mwezi January mwaka ujao.