Sonko atao tahadhari kwa makundi wanaovurugha jitahada zake za kutoa huduma bora

Gavana wa Nairobi  Mike Sonko  ametoa tahadhari kwa makundi kwenye makao makuu ya  kaunti hiyo ambayo anadai yanavurugha  jitihada zake za kutoa huduma bora kwa  umma. Sonko anadai kwa miezi michache ambayo amekuwa Gavana, ameweza  kutambua  na kuwafuta kazi  mafisa kadhaa wafisadi  ambao wamekuwa wakishirikiana na wanachama wa makundi hayo  kuiba fedha za umma. Akiongea  wakati wa kufunguliwa kwa juma la  kutoa uhamasishaji kuhusu ugatuzi hapa jijini Nairobi,Gavana huyo hata hivyo alisema hatua kali ambazo zimechukuliwa kukabiliana na ufisadi zimeanza kufua dafu. Alisema ameagiza idara husika kukabiliana na umwagaji   wa   taka   kando ya barabara za jiji na kwenye  viwanja.

Wakati huo huo,  Sonko  alipongeza baraza la magavana kwa kuandaa  shughuli hiyo  ya kwanza ya uhamasishaji kuhusu ugatuzi  ilioanza leo na ambayo itakamilika Ijumaa hapa jijini. Lengo la shughuli hiyo ni kuuhamasisha umma kuhusu   ufanisi na changamoto za ugatuzi.