Mahakama yatupilia mbali ombi la gavana wa Nairobi Sonko

Mahakama kuu imetupilia mbali ombi la gavana wa kaunty ya Nairobi Mike Sonko la kutaka kesi ya kupinga ushindi wake itupiliwe mbali.jaji wa mahakama kuu Msagha Mbogholi alisema dai la sonko kwamba ni lazima pia naibu wake Polycarp Igathe ashirikishwe kwenye kesi hiyo halina msingi wowote.Uamuzi huo unamaanisha kwamba kesi hiyo itaendelea.Kesi hiyo iliwasilishwa na wapiga kura wawili Japheth Muroko na Zacheus Okoth kwa madai kwamba uchaguzi mkuu wa tarehe nane mwezi agosti ulikumbwa na kasoro.Sonko alimshinda Evans Kidero ambaye jaribio lake la kushirikishwa kwenye kesi hiyo lilitupiliwa mbali na mahakama mwezi uliopita.