Sonko adai agizo lake la kuhamisha vituo vya matatu kati kati mwa jiji limeingizwa siasa

Gavana wa Nairobi Mike Sonko sasa anadai kuwa agizo lake la kuhamisha vituo vya Matatu kutoka kati-kati mwa jiji ili kupunguza msongamano limeingizwa siasa. Sonko ameelezea kwa ufasaha kwa kutuma taarifa na videoA�kuelezea ilani yake iliyochapishwa kwenye gazeti rasmi la serikali kuhusu kuhamishwa kwa vituo vya matatu iliyotolewa Ijumaa iliyopita itakayoanza kutekelezwa Septemba 20, mwaka huu. Wakati huo huo; maagizo hayo mapya yanaendelea kuibua hisia tofauti miongoni mwa wadau. Sonko anapendekeza kuzinduliwa barabara mpya za kutumiwa kutoka maeneo ya mashariki, kusini na magharibi mwa jiji na barabara ya Thika hadi sehemu muhimu kama vile hospitali kuu ya Kenyatta na kituo cha reli ya kisasa huko Syokimau na Mlolongo bila kuingia eneo la kati-kati mwa jiji. Hata hivyo baadhi ya wakazi wa jiji wameeleza wasiwasi kuhusu usalama wao kutokana na kuhamishwa kwa vituo vya matatu, kutoka eneo la kati-kati mwa jiji.