Sonko aahirisha agizo la kupiga marufuku matatu kati kati mwa Jiji

Wasafiri jijini jana walipata afueni ya muda baada ya gavana wa Nairobi Mike Soko kuahirisha agizo la kupiga marufuku magari ya uchukuzi wa umma kufika kati kati mwa jiji. Gavana huyo wa Nairobi badala yake aliwapa wadau muda wa mwezi mmoja kujiandaa kwa utekelezaji agizo hilo huku akionya kwamba serikali yake haitaruhusu ghasia na vurugu katika jiji kuu. Serikali ya kaunti ya Nairobi siku ya Ijumaa ilitoa ilani ya kuzuia magari ya uchukuzi wa umma kufika eneo la kati-kati mwa jiji kuanzia siku ya Jumatano wiki hii. Kwenye ilani iliyochapishwa katika gazeti rasmi la serikali na kutiwa saini na kaimu katibu wa jiji, Leboo ole Morintat, serikali ya kaunti ilitangaza hatua madhubuti za kupunguza msongamano wa magari jijini. Kwenye agizo hilo, matatu zinazosafiri hadi jijini kutoka barabara ya Waiyaki, Uhuru Highway, Kipande Road na Limuru Road zilitarajiwa kuwachukua abiria na kuwashusha katika kituo cha A cha Fig Tree kwenye barabara ya Muranga��aA� ilhali wanaosafiri kwenda jijini kutoka barabara ya Thika, Kiambu hadi kufikia Ruiru pia walitarajiwa kutumia kituoA� cha Fig Tree B. Matatu zote zinazosafiri kutoka barabara ya Mombasa na Langata ziliagizwa kutumia kituo cha Hakati, ilhali kituo cha reli kilitarajiwa kutumiwa na magari kutoka barabara ya Ngong. Kituo cha Muthurwa kilitarajiwa kutumiwa na magari kutoka barabara ya Jogoo na Lusaka, ilhali kituo cha Machakos kilitarajiwa kutumiwa na magari kutoka mashambani.