Simba Waonekana Wakiranda Kwenye Barabara Za Ngong

Shirika la uhifadhi wa wanyama pori nchini-KWS linatoa witokwa yeyote ambaye huenda amewaona simba wawili wakirandaranda kwenye barabara ya Ngong kuwasiliana na shirika hilo kupitia nambari 0800 597 000 au kutuma barua pepe kupitia kwa communications@kws.go.ke. Inadaiwa wanyama hao walionekana wakitembea karibu na ua unaozingira msitu wa Ngong kwenye makutano ya barabara kuelekea Karen na barabara ya Southern Bypass karibu na uwanja wa huduma za kitaifa za misitu. Afisa wa mawasilino wa shirika la huduma kwa wanyama pori nchini Paul Udoto kwenye taarifa kwa vyumba vya hbari alisema polisi wa trfiki wanaoshika dori kwenye barbara hiyo leo mwendo wa saa nne asubuhi waliwaona samba hao na kufahamisha mbuga y taifa ya wanyama pori ya Nairobi. Kundi la maafisa wa shirika la KWS kwa sasa liko eneo hilo kuwasaka simba hao.