Siku ya wanawake yaadhimishwa kote ulimwenguni

Wakenya kote nchini wamejiunga na ulimwengu kuadimisha  siku kuu ya   kimataifa ya wanawake.   Mada kuu ya maadhimisho ya mwaka huu ni ‘Piganieni Ustawi’  na yameleta pamoja  serikali za  mataifa, mashirika ya wanawake, kampui za kibiashara na  mashirika ya wanawake.  Na huku ulimwengu ukiadimisha siku hiyo, jamii ya WaSamburu imeommbwa iwaaelimishe watoto wa kike  ili  iwe na viongozi wengi wa kike mnamo siku za usoni.   Wakiongea alipozuru gereza la Maralal  kuadimisha siku kuu ya  kimataifa  ya wanawake, viongozi wa eneo hilo  waliwahimiza wanawake  kuwa  wanyenyekevu  wanapopiga hatua zaidi.  Wakiongozwa na mwakilishi maalum  wa wadi, Antonnela Loburia, viongozi hao waliitaka serikali ya kaunti hiyo  kuwapa wanawake kandarasi zaidi.  Katika kaunti ya  Kiambu,  mwakilishi wa wanawake katika sehemu hiyo Gathoni wa Muchomba  alisikitishwa na   visa  vingi vya ghasia za kijinsia. Muchoma ambaye alikuwa amezuru  Hospitali ya  Level Five ya Kiambu, aliwataka wanawake kutonyamaza wanapoathirika  na  visa hivyo.  Hatimaye aliwapa visodo wanawake waliokuwa kwenye wadi za kujifungua. Siku Kuu  ya Kimataifa ya wanawake huadimishwa kote ulimwenguni  huku ikiangazia hatua ambazo wamepiga kwenye maswala ya kijamii,uchumi, utamaduni na siasa.  Siku hiyo pia hutoa fursa ya kuangazia mikakati ya kuleta usawa wa jinsia.