Siku Ya Mwisho Ya Kutuma Maombi Ya Kuwania Wadhifa Wa Jaji Mkuu Ni Ijumaa Tarehe 8 Mwezi huu

Tume ya kuajiri maafisa wa idara ya mahakama imeongeza kwa siku moja zaidi, muda wa kupokea maombi ya wanaowania wadhifa wa jaji mkuu kutoka kesho tarehe-7 hadi ijumaa tarehe-8 mwezi huu saa kumi na moja jioni. Msajili mkuu wa idara ya mahakama, Anne Amadi amesema makataa hayo yameongezwa baada ya siku ya alhamisi kutangazwa kuwa siku kuu ya Eid-ul-Fitr. Hata hivyo, Amadi ambaye pia ni katibu wa tume ya JSC amefafanua kuwa muda wa kutuma maombi ya kuwania wadhifa wa naibu jaji mkuu hautabadilika huku tarehe ya mwisho ikisalia kuwa leo jumatano. Wadhifa wa jaji mkuu ulibaki wazi baada ya kustaafu mapema kwa Dr Willy Mutunga mwezi uliopita. Anayetuma maombi ya kuwania wadhifa wa jaji mkuu sharti awe amehudumu kama jaji wa mahakama kuu au mahakama ya rufani kwa kipindi cha miaka-15.