Upinzani Wajadili Jinsi Ya Kushinda Uchaguzi Ujao

Viongozi wa upinzani wamekongamana katika kituo cha Bomas kutafakari kuhusu muungano wa upinzani kabla ya uchaguzi mkuu wa mwezi agosti. Vinara wa muungano wa CORD, Raila Odinga, Kalonzo Musyoka na Moses Wetangula wanatarajiwa kujumuika na kiongozi wa chama cha Amani National Congress, Musalia Mudavadi na kutoa tangazo kwa wafuasi wao kuhusu uwezekano wa kubuni muungano madhubuti kwa lengo la kutwaa uongozi kutoka mrengo wa Jubilee. Viongozi waliochaguliwa walianza kuwasili kwenye kituo hichoA� leo asubuhi. Viongozi hao pia wanatarajiwa kujadili marekebisho ya sheria za uchaguzi iliyotiwa sahihi hivi majuzi.