Sicily Kariuki atetea uamuzi wa kuwaajiri madaktari kutoka Cuba

Waziri wa afya Sicily Kariuki ametetea uamuzi wa kuwaajiri madaktari kutoka Cuba na kuwahimiza Wakenya kutoingiza siasa katika swala hilo.Wito wake unafwatia malalamiko kutoka kwa baadhi ya wahudumu wa afya hapa nchini waliohoji nia ya hatua hiyo,ilhali kuna maelfu ya Wakenya A�ambao hawana kazi .Maafisa wa chama A�cha madaktari hapa nchini wameitaka serikali inapowaajiri madaktari kutoka nje kushughulikia uhaba uliopo ,kukumbuka kwamba kuna zaidi ya madaktari 1,200 ambao hawajaajiriwa .Akitetea uamuzi huo,waziri alisema madaktari hao 100 kutoka Cuba watasaidia kuboresha huduma ya afya hapa nchini,ambayo ni moja ya ajenda nne kuu za serikali.Akiongea huko Nyeri ,akiwa kwenye ziara ya kukagua vituo vya afya,waziri alisema hata kama madaktari wote waliohitimu hapa nchini wataajiriwa,bado kutakuwa na upungufu,na akatoa wito kwa serikali za kaunti kuaajiri madaktari zaidi ili kuboresha huduma za afya.