Sicily Kariuki akanusha madai ya kuwania wadhifa wa uchaguzi

Waziri wa vijana na maswala ya jinsiaA� Sicily Kariuki amekanusha habari kwamba anapania kuwania wadhifa wa uchaguzi katika kaunti ya Nyandarua au ile ya Embu.Alitaja habari hizo kuwa propaganda akisema hana niya ya kuwani wadhifa wowote wa kisiasa.Akiongea hukoA� Nyandarua ambapo alikutana na makundi mbali mbali pamoja na wadau kujadili shughuli ya usajili wa wapiga kura ,waziri huyo alisema yeye anawashawishi tu wakazi wa maeneo hayo mawili kujiandikisha kama wapiga kura ili waweze kutekeleza haki yao ya kidemokrasia ya kupiga kura.Waziri huyo alikutana na wawaniaji wa nyadhifa mbali mbali za kisiasa ,viongozi wa vijana pamoja na wale wa makanisa ambapo aliwahimiza kuwashawishi wakazi kujisajili kama wapiga kura kabla ya kukamilika kwa muda wa shughuli hiyo