Jubilee na Cord Wazozana Kuhusu IEBC

Baadhi ya wabunge wa chama cha Jubilee wanataka tume huru ya uchaguzi na mipaka (IEBC) kulipa bunge maelezo ya kina kuhusu ufadhili wa wadhamini kufikia wiki ijayo. Wakiongozwa na kiongozi wa wengi katika bunge la taifa Aden Duale, wamesema wamemwomba mwenyekiti wa kamati ya haki na maswala ya kisheria kushurutisha tume ya IEBC kutoa maelezo kuhusu rasil-mali zote ambazo vyama vya kisiasa vimepokea kutoka kwa wadhamini na serikali za kigeni kabla ya uchaguzi mkuu mwakaA� 2017.

Akiongea katika makao makuu ya chama hicho jijini Nairobi, Duale vile vile alisema upinzani unapanga njama ya kuiba kura katika uchaguzi mkuu ujao. Alisema hatua ya kiongozi wa upinzani Raila Odinga ya kusisitiza utumiaji wa mitambo ya kusajili wapiga kura kwa njia ya kielektroniki (BVR) inazua shaka.

Duale pia alipuzilia mbali madai kuwa chama cha Jubilee kinalenga kushawishi matokeo ya uchaguzi mkuu mwakaA� 2017 kupitia mswada wa marekebisho yaA� sheria za uchaguzi akisema marekebishoA� yananuiwa tu kupendekeza njia mbadala za kuandaa uchaguzi huo iwapo mfumo wa dijitali utafeli katika baadhi ya sehem