Siasa Kaunti Ya Kajiado

A�Lenku (1)A�

Aliyekuwa waziri wa usalama wa kitaifa, Joseph Ole Lenku ameidhinishwa na wazee wa jamii ya Wa-Maasai kuwania wadhifa wa gavana wa Kajiado, hali ambayo huenda ikabadili mwelekeo wa siasa katika kaunti hiyo. Wanachama-15 wa kundi la wazee wa jamii hiyo almaarufu,A�Iseuri kutoka wadi-25 za kaunti hiyo, walikusanyika katika kijiji cha Olokii huko Loitokitok kwa shughuli hiyo.

Wazee hao wakiongozwa na Jon ole Somiti, waliandaa maombi ya kiasili ambapo walimnyunyizia Ole Lenku maziwa kama njia ya kumbariki na kumuidhinisha kuwania wadhifa wa gavana wa Kajiado katika uchaguzi mkuu ujao.

Zaidi ya wanachama wanane wa bunge la kaunti hiyo walihudhuria hafla hiyo. Walidai kwamba Ole Lenku ndiye anayefaa zaidiA�kugombea kiti hicho.

Kwa upande wake, Ole Lenku alisema hatua ya wazee hao ni ishara kwamba wana imani naye. Alitoa wito wa umoja, akisema ana imani ataibuka mshindi katika uchaguzi huo.

Katika siku za hivi majuzi, Ole Lenku amekuwa akitofautiana na mrithi wake Joseph Nkaissery ambaye yaonekana anamuunga mkono mgombeaji mwingine.