Shule Za Chekechea Kupokea Mtandao Nyamira

Serikali ya kaunti ya Nyamira imejumuisha elimu kwa njia ya mtandao kwenye elimu ya chekechea ili kuwavutia watoto zaidi kwenye vituo vya umma. Shule 11 za sekondari katika kaunti tano ndogo zitakuwa vituo vya elimu kwa njia ya mtandao ili kuwasaidia walimu wa shule za chekechea kufanya utafiti huku serikali ya eneo hilo ikitafuta washirika ili kuimarisgha mpango huo. GavanaA� John Nyangarama aliyasema hayo alipozindua usambazaji wa vifaa vya mafunzo na masomo kwa vituo vyote vya elimu ya chekechea kwenye kaunti hiyo. Nyangarama aliwaagiza maafisa wanaosimamia idara hiyo pamoja na shule binafsi kuhakikisha kwamba vifaa hivyo vinatumiwa kwa njia ifaayo. Alisema kuwa serikali ya kaunti hiyo tayari imewaajiri zaidi ya walimu 800 wa shule za chekechea na kujenga madarasa 20. Vifaa hivyo vitasambazwa kwenye vituo katika wadi zote 20 kulingana na idadi ya wanafunzi. Vifaa hivyo ni pamoja na meza, viti vya walimu na watoto, vitabu vya kuandikia, kalamu, penseli, penseli za rangi, silabasi na faili.