Shule ya Highway yafungwa

Shule ya Sekondari ya Highway iliyoko mtaa wa South B Jijini Nairobi, imefungwa kwa muda usiojulikana kufuatia kisa cha moto kwenye bweni moja Jumapili asubuhi. Moto huo ulinzia katika orofa ya kwanza ya bweni hilo lakini ulizimwa na wanafunzi wakishirikiana na waalimu. Shirika la msalaba mwekundu nchini linasema wanafunzi 12 walikimbizwa hospitalini kufuatia kisa hicho. Chanzo cha moto huo ambao unafuatia visa vingine vya moto katika zaidi ya shule 47 kote nchini hakijajulikana. Kulingana na shirika la msalaba mwekundu nchini, hospitali kuu ya Kenyatta iliwatibu wanafunzi hao kutokana na majeraha madogo madogo, na pia hali ya kuvuta hewa yenye moshi.