Shule 150 Nchini Kunufaika Na Mpango Wa Vipakatalishi Katika Awamu Ya Kwanza

Wizara ya elimu imezindua awamu ya kwanza ya kutoa vipakatalishiA� kwa wanafunzi wa darasa la kwanza katika shule 150A� katika maeneo mbali mbali hapa nchini . Akizindua mpango huo jana katika shule ya msingi ya Kiambu,kwenye kaunti ya Kiambu,waziri wa elimu Dr. Fred Matianga��i alisema chini ya mpango huo,wanafunzi wa darasa la kwanzaA� katika shule zote za msingi za umma watapokea mtaala wa masomo kupitia vifaa hivyo. Alisema serikali imetumia shilling million 200 katika kipindi cha mwaka 2016/2017 kuweka muundo mbinu wa kufanikisha mpango huo .Waziri alisema hiyo inashirikiana na ile ya teknolojia ya mawasiliano kutekeleza mpango huo .Aliongeza kuwa serikali tayari imeanza kutoa mafunzo kwa walimu kuwaanda kwa mpango huo wa dijitali .