Shughuli zakwama Caracas mji mkuu wa Venezuela kufuatia mgomo

Shughuli katika maeneo kadha ya mji mkuu wa Venezuela, zilikwamishwa hapo jana huku wapinzani wa Rais Nicolas Maduro wakiitisha mgomo muhimu wa kwanza tangu ule wa mwaka 2002 ambao ulishindwa kumnga��oa mamlakani mtangulizi wa Maduro, Hugo Chavez. Mgomo huo wa sekta ya uchukuzi wa Umma A�ulionekana kukwamisha huduma zote za ma-Bus huku maelfu ya wafanyibiashara wa kibinafsi wakikaidi maagizo ya serikali ya kuendelea na shughuli za kawaida. Hata hivyo kampuni zinazodhibitiwa na serikali ziliacha wazi milango yao, ijapo hakukwua na wafanyikazi.waandamanaji hao walifunga barabara nyingi kwa kuweka vizuizi , huku maafisa wa usalama wakitumia gesi ya kutoa machozi kutawanya wadhibiti wa vizuizi hivyo. Zaidi ya watu 170 walitiwa nguvuni kufikia saa za alasiri kulingana na kundi moja la kutetea haki za binadamu. Mgomo huo wa masaa 24 unalenga kupinga mipango ya rais Maduro, ya kuandaa kura ya maamuzi ili kufanyia katiba marekebisho. Upizani umesema utasusia uchaguzi ambao umepangiwa kufanyika tarehe 30 Julai, ili kuwachagua wabunge wapya.

A�