Shughuli za upigaji kura zaanza rasmi katika kaunti ya Migori

Shughuli ya upigaji kura  kumchagua seneta mpya katika kaunti ya Migori ilianza leo alfajiri chini ya ulinzi mkali.Kamanda wa polisi wa kaunti hiyo Joseph Nthenge amesesma kila kituo cha kupigia kura kati ya vituo 826 vilivyopo katika kaunti hiyo kimewekewa usalama na maafisa wawili wa polisi.

Pia amesema maafisa wake watahakikisha sheria, utulivu na amani vinadumishwa wakati wa upigaji kura na shughuli ya kuzihesabu.Nthenge amesema kwamba wametambua maeneo yaliyo hatari kwa ghasia na kwamba wamewapeleka maafisa zaidi kushika doria kwenye maeneo hayo.

Migori ilikumbwa na ghasia wakati wa kampeini na uchaguzi ingawa vurugu chache ziliripotiwa wakati wa kampeini za uchaguzi huo mdogo. Kinyang’anyiro cha useneta cha Migori kinaonekana kuwa kati ya mgombea wa chama cha ODM  Ochillo Ayacko mgombea wa chama cha Federal Party of Kenya Eddy Oketch. Kuna wagombea watano wanaowania kiti hicho.