Shughuli ya uteuzi wa chama cha Jubilee kaunti ya Nairobi yaahirishwa

Chama cha Jubilee kimehairisha shughuli yake ya uteuzi katika kaunti ya Nairobi kutoka kesho  ijumaa  hadi siku ya jumatatu tarehe 24 juma lijalo. Katika taarifa, katibu mkuu wa chama hicho  Raphael Tuju  alisema kuwa uamuzi huo uliafikiwa na kamati kuu ya kitaifa ya chama hicho baada ya kushauriana na bodi ya uchaguzi ya chama hicho.  Alisema kuwa chama hicho kitafanya shughuli hiyo kwa siku mbili baada ya kuongezeka kwa idadi ya kaunti ambapo shughuli hiyo inatarajiwa kuandaliwa.  Chama hicho awali kilikuwa kimepanga kuandaa shughuli hiyo kesho kwa siku moja.